Kwa kuanza na mofolojia, wataalamu mbalimbali wamefasili
mofolojia kama ifuatavyo,
Massamba na wenzake (2009:32) wanafasili mofolojia kuwa
ni kiwango cha sarufi kinachojishughulisha na uchambuzi wa mfumo wa maneno
katika lugha yaani jinsi maneno ya lugha yoyote iwayo inaundwa.
Besha (2007:49) anasema mofolojia ni taaluma
inayojishughulisha na kuchambua muundo wamaneno katika lugha. Misingi ya
wataalamu hawa wawili wanaonekana kuingiliana katika kuonyesha namna ya taaluma
ya mofolojia inavyojihusisha na muundo wa maneno katika lugha. Mofimu ndio
kipashio cha msingi katika mofolojia.
Pia Lubanza (1996:1) anaonekana kuungana nao kwa kusema
mofolojia kuwa ni taaluma inayoshuhulika na vipashio vya lugha na mpangilio
wake katika uundaji wa maneno.mtaalamu anaongezea namna vipashio vinavyotumika
katika kupangilia mfumo wa muundo wa maneno katika lugha. Kipashio cha msingi
katika mofolojia ni mofimu.
Hivyo
basi fasili ya mofolojia imeonekana kugusia uundaji wa maneno katika lugha kwa
mpangilio maalumu. Hivyo mofolojia inaweza kuelezwa kwamba ni taaluma
inayoshughulika na uchunguzi na uchambuzi wa maumbo mbalimbali ya maneno katika
lugjha.
Baada ya kuangalia
taaluma ya mofolojia, kuna wataalamu mbalimbali ambao wamefasili dhana ya
fonolojia, wataalamu hao nia kama wafuatao.
Habwe
na Karanja (2007:42) wanafafanua fonolojia kuwa ni taaluma inayoshughulika
jinsi sauti zinavyotumika, zinavyounganishwa na kupangwa katika lugha yoyote
mahususi ili kuunda tungo zenye maana. Wanaeleza kuwa sauti hizo zinazotumika katika lugha hiyo mahususi
hujulikana kama fonimu.
TUKI (2004) wanaifasili
fonolojia kuwa ni tawi la isimu ambalo linajishughulisha na uchambuzi wa mfumo
wa sauti katika lugha.
Vilevile
Kihore ne wenzake (2004:6) wanafasili fonolojia kuwa ni tawi la isimu ambalo
hujishughuliah na uchunguzi, uchambuzi na uainishaji wa sauti pambanuzi ambao
hutumika katika mifumo mbalimbali ya sauti za lugha za binadamu. Katika
fonolojia kipashio cha msingi kinachohusika ni fonimu.
Kwa
ujumla fasili zilizoelezwa hapo juu ni za msingi katika taaluma ya fonolojia
kwani wataalamu wote wanaelekea kukubaliana kuifasili fonolojia kuwa ni ni
uwanja waisimu unaojisgughulisha na
uchunguzi na uchambuzi wa sauti za lugha mahususi.
Kimsingi taaluma ya
mofolojia na fonolojia hufanana na kuhitilafiana kwa kiasi kikubwa. Ifuatayo ni
maelezo kuhusu ufanano wa fonolojia na mofolojia.
Kwanza,
vipashio vya kifonolojia ndivyo vinavyouna vipashio vya kimofolojia, kwa
kutumia fonimu ambacho ndio kipashio cha msingi katika fonolojia huweza kuunda
mofimu ambayo ndiyo kipashio cha msingi cha kimofolojia.