Wednesday, December 25, 2013

Kufanana na kuhitilafiana kwa mofolojia na fonolojia




                                                                                                                     
Katika kujadili swali hili tutaanza kufasili dhana kuu zilizojitokeza ambazo ni fonolojia na mofolojia. Ambapo wataalamu mbalimbali wamefasili dhana hizi huku kila mmoja akitoa fasili yake. Pia tutatalii kwa kina juu ya kuhitilafiana na kufanana kwa fonolojia na mofolojia na mwisho ni hitimisho.
             
Kwa kuanza na mofolojia, wataalamu mbalimbali wamefasili mofolojia kama ifuatavyo,

      Massamba na wenzake (2009:32) wanafasili mofolojia kuwa ni kiwango cha sarufi kinachojishughulisha na uchambuzi wa mfumo wa maneno katika lugha yaani jinsi maneno ya lugha yoyote iwayo inaundwa.

             Besha (2007:49) anasema mofolojia ni taaluma inayojishughulisha na kuchambua muundo wamaneno katika lugha. Misingi ya wataalamu hawa wawili wanaonekana kuingiliana katika kuonyesha namna ya taaluma ya mofolojia inavyojihusisha na muundo wa maneno katika lugha. Mofimu ndio kipashio cha msingi katika mofolojia.
 
            Pia Lubanza (1996:1) anaonekana kuungana nao kwa kusema mofolojia kuwa ni taaluma inayoshuhulika na vipashio vya lugha na mpangilio wake katika uundaji wa maneno.mtaalamu anaongezea namna vipashio vinavyotumika katika kupangilia mfumo wa muundo wa maneno katika lugha. Kipashio cha msingi katika mofolojia ni mofimu.

Hivyo basi fasili ya mofolojia imeonekana kugusia uundaji wa maneno katika lugha kwa mpangilio maalumu. Hivyo mofolojia inaweza kuelezwa kwamba ni taaluma inayoshughulika na uchunguzi na uchambuzi wa maumbo mbalimbali ya maneno katika lugjha.
Baada ya kuangalia taaluma ya mofolojia, kuna wataalamu mbalimbali ambao wamefasili dhana ya fonolojia, wataalamu hao nia kama wafuatao.

Habwe na Karanja (2007:42) wanafafanua fonolojia kuwa ni taaluma inayoshughulika jinsi sauti zinavyotumika, zinavyounganishwa na kupangwa katika lugha yoyote mahususi ili kuunda tungo zenye maana. Wanaeleza kuwa sauti hizo  zinazotumika katika lugha hiyo mahususi hujulikana kama fonimu.

TUKI (2004) wanaifasili fonolojia kuwa ni tawi la isimu ambalo linajishughulisha na uchambuzi wa mfumo wa sauti katika lugha.

Vilevile Kihore ne wenzake (2004:6) wanafasili fonolojia kuwa ni tawi la isimu ambalo hujishughuliah na uchunguzi, uchambuzi na uainishaji wa sauti pambanuzi ambao hutumika katika mifumo mbalimbali ya sauti za lugha za binadamu. Katika fonolojia kipashio cha msingi kinachohusika ni fonimu.

Kwa ujumla fasili zilizoelezwa hapo juu ni za msingi katika taaluma ya fonolojia kwani wataalamu wote wanaelekea kukubaliana kuifasili fonolojia kuwa ni ni uwanja waisimu unaojisgughulisha na  uchunguzi na uchambuzi wa sauti za lugha mahususi.
Kimsingi taaluma ya mofolojia na fonolojia hufanana na kuhitilafiana kwa kiasi kikubwa. Ifuatayo ni maelezo kuhusu ufanano wa fonolojia na mofolojia.

Kwanza, vipashio vya kifonolojia ndivyo vinavyouna vipashio vya kimofolojia, kwa kutumia fonimu ambacho ndio kipashio cha msingi katika fonolojia huweza kuunda mofimu ambayo ndiyo kipashio cha msingi cha kimofolojia.

Dhana ya mtindo na nafasi yake katika fasihi.


 
Kabla hatujaangalia dhana ya mtindo ni vema tukajua kwanza dhana ya fasihi.

Wataalamu wengi  akiwamo Wamitila (2003) wanakubaliana kuwa fasihi ni sanaa inayotumia lugha na ambayo hujishughulisha na binadamu pamoja na maisha yake na huathiri, hugusa, au huacha athari Fulani na hupatikana katika umbo ambalo linatambuliwa na jamii. Kwa ujumla fasihi ni sanaa inayotumia lugha na yenye maudhui katika jamii husika.

Baada ya kuangalia dhana ya fasihi kwa ujumla sasa tuangalie dhana ya mtindo na nafasi yake katika fasihi.

Senkoro (1982) anasema mtindo katika kazi ya fasihi ni ile namna ambayo msanii hutunga kazi hiyo na huipa sura ambayo kifani na kimaudhui huainisha kanuni au kawaida zilizofuatwa (za kimapokeo) ama ni za kipekee. Anaendele kusema, mtindo ni upangaji wa fani na maudhui katika kazi ya fasihi kwa njia ambayo hutokeza au huonyesha nafsi na labda upekee wa mtungaji wa kazi hiyo.

Katika fasili hii tunaweza kuona anachokieleza mtaalamu huyu ni kwamba mtindo huhusiha upangaji wa fani na maudhui katika kazi ya fasihi ambapo upangaji huu hutegemea upekee alionao msanii. Kwa maana nyingine, unaposoma kazi Fulani ya fasihi unaweza kumwona mtunzi wa kazi hiyo kulingana na jinsi alivyoiandika, kwa maana kwamba jambo moja linaweza kuongelewa na wasanii wawili tofauti lakini namna linavyowasilishwa likatofautiana na hii ni kulingana na upekee wao.

Wamitlia (2003) naye anasema “mtindo ni jumla ya mbinu au sifa zinazomwezesha mwandishi kuwasilisha ujumbe  wake. Huelezea mwandishi anavyounda kazi yake “. Anaendelea kusema, dhana ya mtindo hurejelea sifa maalumu za mwandishi au mazoea ya mwandishi Fulani ambayo hujionyesha kwenye fani yake, mazoea hayo ya mwandishi ya kuandika, kuteua msamiati, tamathali za semi, taswira, uakifishi, sentensi na kadhalika ndio yanayompambanua mwandishi huyu na mwanzake.


JINSI MWANDISHI WA KAZI ZA FASIHI ZA WATOTO NA VIJANA ANAVYOPASWA KUZINGATIA SAIKOLOJIA YA WATOTO NA VIJANA: UCHAMBUZI KUTOKA KATIKA KITABU CHA MWENDO.



Fasihi ni sanaa kama zilivyo sanaa zingine, mvuto ni kitu cha msingi sana katika sanaa. Fasihi ya watotona vijana pia kama sanaa ni muhimu pia kuzingatia kipengele hiki. Kwa mantiki hii, mwandishi ili aweze kufanikisha kuiteka saikolojia ya watoto na vijana katika kazi yake ni lazima ahakikishe kazi hiyo inamvuto kwa watoto. Dhana ya mvuto katika fasihi ya watoto na vijana inahusisha vipengele kadhaa, kabla ya kuangalia vipengele hivi kwa kina ni vema tukafasili dhana muhimu zinazojitokeza katika swali. Dhana hizo ni pamoja na Fasihi ya watoto na vijana na dhana ya saikolojia ya watoto na vijana katika kazi za fashi. Baada ya kuangalia dhana hizi kwa kina ndiposa tutahusianisha na riwaya ya “Mwendo”.

Kwa mujibu wa Wamitila (2003) Fasihi ya watoto ni fasihi maalum inayoandikwa kwa ajili ya watoto.

NOUN (2010) Wanasema Fasihi ya watoto ni dhana inayorejelea fasihi inayowalenga watoto pekee. Wanaendelea kusema, Fasihi ya watoto huweza kuwa hadithi, ushairi, visakale, drama ambazo zimetungwa kwa ajili ya watoto wadogo na vijana. Vilevile wanaongezea kusema kuwa Fasihi ya watoto inajikita katika mambo makuu matatu, jambo la kwanza ni endapo mhusika mkuu ni mtoto au kijana, dhamira inayowahusu watoto na lugha rahisi na Fasihi ya watoto inakuwa fasihi ya watoto endapo tu wazo na dhamira inahusiana na urahisi wa lugha.

Fasili zote hizi,zinatupa mwanga hasa juu ya dhana ya fasihi ya watoto na vijana, vitu vya msingi ni kwamba fasihi hii ni lazima iwe na dhamira pamoja na lugha rahisi. Hivyo basi, tunaweza kusema kuwa, fasihi ya watoto na vijana ni sanaa itumiayo lugha kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa hadhira iliyo chini ya umri wa miaka kumi na minane (18).

Dhana ya saikolojia ya watoto na vijana tunaweza kusema ni yale mambo ambayo yanatakiwa kuzingatiwa katika kazi za Fasihi ili kumvutia mtoto na kijana. Sigh na wenzake (2002) wanasema Fasihi ya watoto na vijana lazima iwe inaonesha matendo na maisha ya mhusika kinaganaga, mhusika awe anatia hamasa na lazma iwe inaburudisha.

Kwa ujumla saikolojia ya watoto na vijana katika kazi za fasihi hulenga yale mambo ambayo ni lazima yawepo katika kazi hiyo ili kuwavutia watoto na vijana. Kwa hiyo ili mwandishi afanikiwe kuiteka saikolojia ya watoto na vijana ni sharti azingatie mambo hayo, mambo hayo ni pamoja na haya yafuatayo:

Sunday, December 8, 2013

Tofauti nyeti za kimaana za maneno; Chapa, charaza, tandika, zaba, nasa, kafua, nyuka,kung’uta, twanga, timba. (katika muktadha wa kitendo cha kumpiga mtu kwa kumwadhinu) kwa kuzingatia madai ya wataalam kwamba hakuna sinonimia kuntu katika lugha yoyote ile



Katika kuangalia mjadala huu tutaanza kuelezea maana ya sinonimia kwa mujibu wa wataalamu kisha tutaonesha maana za msingi za maneno katika data kwa mujibu wa kamusi, tutabainisha na kufafanua kanuni za msingi za kubainisha sinonimia kuntu, tutazijaribu sinonimia hizo kwa kuzitungia sentensi na kisha kubadilisha nafasi ya kila sinonimia katika kila sentensi na mwisho kabisa tutatoa hitimisho.

Kwa mujibu wa Habwe na Karanja (2004) sinonimia ni visawe vya dhana moja. Kwa ufafanuzi juu ya maelezo haya tunaweza kusema kuwa sinonimia ni maneno tofauti yanayobeba dhana inayofanana. Kimsingi fasili hii inajitosheleza kwani tunaposema sinonimia tuna maana kwamba maneno yenye maana sawa au inayokaribiana. Maneno kuwa na maana sawa au inayokaribiana maana yake ni kwamba maneno haya hurejelea dhana moja.

Kabla hatujaanza kupima sinonimia hizi katika sentensi ni vema tukaangalia maana za msingi za maneno haya. Kwa mujibu wa kamusi ya Kiswahili sanifu maneno haya yana maana zifuatazo:

Dhana ya Lugha kienzo na umuhimu wake katika utengenezaji wa kamusi



Katika kujadili mada hii tutaangalia dhana ya lugha kienzo kama ilivyojadiliwa na wataalamu mbalimbali, mifano ya lugha kienzo kutoka katika kamusi, umuhimu wa lugha kienzo na mwisho tutatoa hitimisho juu mada hii.

Dhana ya lugha kienzo imejadiliwa na wataalamu mbalimbali, miongoni mwa wataalamu hao ni pamoja na:

Bwenge (1995) kama alivyonukuliwa na Mdee (1997) wanasema kuwa lugha kienzo ni lugha au ni mtindo utumikao kufasili au kueleza leksimu za lugha. Kwa kifupi lugha kienzo ni lugha itumikayo kuifafanua au kuifasili lugha. Anaendelea kusema dhima ya lugha za lugha kienzo ni: kueleza lugha kwa ufasaha, utoshelevu , kwa muhtasari na uwazi ili kumwezesha  mtumiaji kupata na kuelewa mara moja kile anachokitafuta bila kumchosha akili.

Fasili hii inaelezea dhana ya lugha kienzo kwa ujumla katika lugha,  lakini hata hivyo kamusi nayo ina lugha inayotumiwa kuelezea taarifa mbalimbali zinazohusu kidahizo ambazo huingizwa katika kamusi. Lugha hii ndio huitwa lugha kienzo ya kamusi.

Dhana ya mtindo na nafasi yake katika fasihi



Kabla hatujaangalia dhana ya mtindo ni vema tukajua kwanza dhana ya fasihi.

Wataalamu wengi  akiwamo Wamitila (2003) wanakubaliana kuwa fasihi ni sanaa inayotumia lugha na ambayo hujishughulisha na binadamu pamoja na maisha yake na huathiri, hugusa, au huacha athari fulani na hupatikana katika umbo ambalo linatambuliwa na jamii. Kwa ujumla fasihi ni sanaa inayotumia lugha na yenye maudhui katika jamii husika.

Baada ya kuangalia dhana ya fasihi kwa ujumla sasa tuangalie dhana ya mtindo na nafasi yake katika fasihi.

Senkoro (1982) anasema mtindo katika kazi ya fasihi ni ile namna ambayo msanii hutunga kazi hiyo na kuipa sura ambayo kifani na kimaudhui huainisha kanuni au kawaida zilizofuatwa (za kimapokeo) ama ni za kipekee. Anaendelea kusema, mtindo ni upangaji wa fani na maudhui katika kazi ya fasihi kwa njia ambayo hutokeza au huonyesha nafsi na labda upekee wa mtungaji wa kazi hiyo.

Sunday, August 25, 2013

AINA ZA USHAIRI (BAHARI)




Bahari; hii ni aina mahususi ya  ushairi yenye sifa fulani kiumbo na pengine hata kimaudhui na kimatumizi na zinazoipambanua na aina nyingine ya ushairi.

S.A Kibao (2003)  anasema, ushairi wa Kiswahili umegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni: shairi, utenzi na ngonjeara. Anaendelea kusema, aina zote hizi kanuni zake ni za pamoja isipokuwa utenzi ambao una mpangilio wa namna ya pekee.

S. Robert na Amri Abeid (1954)  wanasema zipo bahari tatu tu za ushairi nazo ni:wimbo, shairi na utenzi.

A.S. Nabhany na wenzake wameainisha bahari 13 za ushairi na kusema kuwa utungo wowote lazima uingie katika bahari mojawapo. Bahari hizo ni hizi zifuatazo:
1.      Ushairi; Ni utenzi wenye mishororo minne na vipande  viwili kila msitari. Kila mstari una mizani 16 na kila kipande kina mizani 8. Maudhui yake yanatokana na jambo lolote lile analoliona mtunzi.

2.      Wimbo; Ni utungo wenye mishororo mitatu kila ubeti na kila mshororo una vipande viwili. Nyimbo nyingi huongelea mapenzi.

3.      Tenzi; Ni utungo wenye vipande vine katika kila ubeti na vina hubadilika kila ubeti isipokuwa kipande cha mwisho. Tenzi nyingi zina mizani nane kila mshororo na nyingine zina mizani 11 na zingine 10.

4.      Inkshafi/Duramandhuma; Imepata jina lake kutokana na utenzi wa Aliinkshafi. Tenzi hizi zina maadili ya kidini japokuwa maudhui yake yanaweza kutumika katika maadili ya kidunia. Kila ubeti una mishororo minne na kila mshororo una mizani 11.

5.      Ukawafi; Hili ni shairi lenye mishororo mitatu au zaidi katika kila ubeti na vipande vitatu katika kila mshororo. Mizani zinaweza zikatofautiana au zikawa sawa.

6.      Wajiwaji/Takhimisa; Una mishororo mitano kila ubeti na mizanai 15 kila mshororo na vipande vitatu katika kila mshororo vina muundo wa mizani 6, 4, 5. Maudhui yake ni ya kidini au kiamisha kwa ujumla, mfano Takhimisa ya Liongo  na tenzi ya Inkshafi.

7.      Hamziya; lipata jina lake kutokana na kaswida ya Hamziya ambao ni utenzi wa kiarabu. Mishororo ya Hamziya ina vipande 3 vya mizani 5, 4, 6

8.      Tiyani-Fatiha;   Ni ushairi wa kidini wa kuomba toba, una mishororo 9 kila ubeti ambayo huweza kutofautiana kwa urefu/mizani.

9.      Utumbuizo; Haina idadi kamili ya mishororo na mizani, urefu wa mstari au mshororo hutegemea pumzi aliyonayo mwimbaji na lengo lake; mfano ni nyimbo za Liyongo kuna tumbuizo.

10.  Wawe; Ni ushairi au wimbo wa kilimo, huimbwa wakati wa kulima au kupanda.

11.  Kimai; Inahusu shughuli za majini, ni bahari ya wavuvi na mabaharia. Idadi ya mishororo na vina si lazima.

12.  Zivindo; Ni ushairi unaofafanua maana za maneno; na kazi yake ni kujifunza lugha na mkuhifadhi lugha.
Mfano: Kata ni kata ya nyoka
             Au kata ya nyweleni
             Kata ya tweka, bandikwayo kichwani

13.  Sama; Neno ‘sama’ ni mahadhi au sauti, hivyo bahari hii hukusanya washairi wote wenye kufuata mahadhi ya kigeni.

Monday, August 19, 2013

NAFASI YA CHAWAKAMA KATIKA KUUNGANISHA VIJANA WA AFRIKA MASHARIKI

Utangulizi
Lugha ya Kiswahili ina historia ndefu hapa Afrika Mashariki kama chombo cha kuunganisha watu wenye tamaduni tofautitofauti tokea enzi za biashara ya utumwa hadi baada ya uhuru. Wafanya biashara wa enzi za utumwa walitumia lugha ya Kiswahili ili kurahisha mawasiliano na kukidhi haja zao za kibiashara, bila kujua, walijikuata wanakieneza Kiswahili kutoka pwani ya Tanganyika hadi bara ya Kongo. Wakoloni nao walipokuja Afrika Mashariki waliona Kiswahili ndio lugha pekee ya kurahisha utawala wao, lakini baadae walikuja kugundua kuwa Kiswahili ilikuwa ni silaha ya kuangamiza utawala wao na hivyo wakahafifisha matumizi ya Kiswahili.

Wanaharakati wa utaifa, wakati wa kupigania uhuru hususani katika nchi ya Tanganyika waliona Kiswahili ndio njia pekee itakayowasidia kupata uhuru bila hata kumwaga tone la damu. Mwalimu Nyerere alitumia fursa hii kuwaunganisha watanganyika wote wenye tamaduni tofautitofauti na waliokuwa wakizungumza lugha tofautitofauti, lakini kwa kupitia lugha ya Kiswahili walikuwa na kauli moja ya kutaka Tanganyika ya watanganyika huru. Umoja huu umedumu hadi leo Tanzania inajulikana kuwa ni nchi ya watu wakarimu na wenye umoja. Isingewezekeana kufukia hapa kama kila mtu angejitukuza kwa kabila lake ila kwa kutumia Kiswahili watanzania sasa ni wamoja, hakuna msamiati katika mazungumzo ya watanzania unaotukuza ukabila.

Wednesday, July 17, 2013

MJADALA KUHUSU IDADI YA LAHAJA ZA KISWAHILI NA NAMNA ZILIVYOINUKIA

Dhana ya lahaja
Dhana ya lahaja ni changamani, hutokana na jinsi mtu aliyefasili dhana hiyo anatumia kigezo kipi. Mfano,  kuna kigezo cha isimujamii, hiki ni kigezo cha kuwashirikisha wanajamii au wazungumzaji wa lahaja hiyo na ukapata msimamo wao kuhusu lahaja hiyo. Pia kuna kigezo cha kiisimu; hiki kigezo cha kutofautisha lugha na lahaja nyingine kwa kutumia vigezo vya msamiati wa msingi, fonolojia, pamoja na mofolojia.

Lahaja pia inaweza kufasiliwa kwa kuzingatia utengano wa kijiografia au kijamii. Hii ana maana kwamba unaweza kusikia kuwa lahaja fulani inazungumzwa mahala fulani au huzungumzwa na kundi la watu fulani. Mfano, lahaja ya kitumbatu huzungumzwa sehemu za kisiwa cha Tumbatu vivyo hivyo lahaja ya kipemba huzungumzwa na watu wa Pemba.

Hebu tuangalie uchangamani wa dhana ya lahaja kwa kuangalia fasili zifuatazo:
 Msanjila (2009:124) anasema lahaja ni lugha mojawapo kati ya lugha ambazo kimsingi kuhesabiwa kuwa lugha moja isipokuwa zinatofautiana katika baadhi ya vipengele fulani fulani kama vile lafudhi, fonolojia, msamiati usiokuwa wa msingi au muundo kutokana na eneo lugha hiyo inazungumzwa.

Massamba (2002) anasema kuwa lahaja ni lugha mbalimbali za pwani zilizokuwa na uhusianao wa karibu sana. Lugha hizo ni kama vile ci-mbalazi, ki-amu, ki-mvita, ki-jomvu, ki-mtang’ata, ki-makunduchi, ki-tumbatu, ki-mgao na ki-unguja. Wakati wengine wanaziita lahaja mfano, Polome (1967), Bryan (1959) pamoja na Temu (1980).

Kwa mujibu wa Wikipedia, Kamusi elezo huru  lahaja ni vilugha vidogo vidogo vya lugha moja ambavyo hubainika kijamii au kijiografia.

Ukizitazama fasili hizi kwa makini utagundu kuwa kila mtu ana mtazano wake kuhusu lahaja, wengine wanasema ni vilugha, ni lugha inayojitegemea, wengine wanasema ni tofauti ndogondogo hasa za kimatamshi katika lugha moja. Lakini pia wengine wanaona lahaja ni tofauti za lugha kwa kigezo cha kijiografia na wengine wanaona ni tofauti za kijamii na kijiografia. Kwa hiyo mitazamo hii ndio hulete utata na uchangamani katika kufasili dhana ya lahaja.

Kimsingi fasili iliyotolewa na Msanjila (keshatajwa) inaweza kutusaidia kujua dhana ya lahaja kwani fasili hii ni ya kiutendaji.Kwa hiyo lahaja ni lugha mojawapo kati ya lugha ambazo kimsingi kuhesabiwa kuwa lugha moja isipokuwa zinatofautiana katika baadhi ya vipengele fulani fulani kama vile lafudhi, fonolojia, msamiati usiokuwa wa msingi au muundo kutokana na eneo lugha hiyo inamozungumzwa.

Mjadala kuhusu idadi ya lahaja za kiswahili na namna lahaja hizi vilivyoinukia:
Mjadala hu ulianza siku nyingi kidogo na hadi sasa hivi hakuna utafiti wa hivi karibuni unaoweza kutusaidia kuthibitisha idadi kamili za lahaji za Kiswahili. Hebu tuangalie wataalam jinsi wanavyojadili idadi ya lahaja za Kiswahili.

Chiraghdin na Mnyampala (1977) wametaja idadi ya lahaja ishirini, lahaja hizo ni kama vile; Kiunguja, Kimrima, Kimgao, Kimvita, Kihadimu, Kipemba, Kirumba, Kiamu, Kipate, Kisiu, Kitikuu, Kingazija, Kingozi, Kitumbatu, Kimtang’ata, Chichifundi, Chibalanzi, Kingwana, Kinyare, na Kijomvu.

Nurse na Spear (1985) wametaja idadi ya lahaja kumi na sita (16), na wamezigawa katika makundi mawili ambayo ni kundi la kaskazini na kundi la kusini. Mfano kundi la kaskazini lina lahaja saba (7) wakati kundi la kusini lina lahaja tisa (9). Baadhi ya lahaja hizo ni;- Kipate, Chimiini, Kibajuni, Kisiu, Kijomvu, Chifunzi, Kipate, Kiunguja, Kimtang’ata, Kimakunduchi na kuendelea.
Utata kuhusu idadi za lahaja za kiswahili unatokana na sababu zifuatazo;

Kigezo kilichotumika katika kufanya utafiti wa lahaja za kiswahili. Unaweza kufanya utafiti wa lahaja za kiswahili kwa kutumia kigezo cha kijiografia, kijamii, pamoja na kiisimu. Vigezo hivyo vyote vinaweza kukupatia idadi tofauti za lahaja mfano, Massamba katika utafiti wake kwa kutumia kigezo cha kiisimu (1977) alifanya utafiti katika jamii za chi-ruri, chi-jita, na ki-kwaya akathibitisha kuwa hizi ni lahaja za lugha moja na si tofauti, pia kwa kutumia kigezo cha utengano wa kijiografia na kijamii mfano katika lugha ya Kiswahili kwa kiasi kikubwa uanishaji umefanywa kwa utengano wa kijiografia kama vile,  kipate kinazungumzwa sehemu za Pate na lahaja ya kipemba huzungumzwa  Pemba. Hivyo kutokana na sababu kama hizi husababisha watafiti wengi kutofautiana katika kupata idadi kamili za lahaja.